tangazo

Thursday, May 5, 2011

Jamii ielimishwe madhara ya nyama isiyokaguliwa

Na Ramadhan Libenanga

MOJAWAPO ya jambo la hatari kwa maisha ya binadamu ni kula chakula bilka kuthibitishwa na wataalam husika.Kundi hatari zaidi kupata maaradhi yanayosabishwa na vyakjula visivyothitishwa na
wataalam ni walaji wa nyama aina zote.

Wataalam wa mifugo wamekuwa wakishauri wana jamii kuwa makini na nyama kwa kuhoji kama imepitiwa na kuthibitishwa na watalaamu kabla ya kununua na kula.Nyama ya ng'ombe,mbuzi na nguruwe (kiti moto) ni vitoweo vinavyopedwa na watanzania wengi hasa watumiaji vileo ili kukamilisha burudani.

Shughuli nyingi za jamii za kitanzania kama vile harusi, misiba,ugeni na mitambiko hutumia zaidi nyama kama vile ng'ombe,mbuni au kondoo.

Wanyama hawa ndio wanyama ambao wamekuwa na mvuto mkubwa kwa walaji lakini siku zote , kumekuwa na msemo unaosema ”kizuri kina madhara “.

Mbuzi na Nguruwe  ni wanyama walio katika kundi la damu moto.Wanyama hawa wanamagonjwa ambayo moja kwa moja yanaweza kumuambukiza mlaji kama haikupitiwa na wataalam wa mifugo.

Hakuna asiye fahamu taratibu na sheria zilizowekwa na Wizara ya Kilimo, Chakuna na Ushirika pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ushirika kuhusu suala  zima la uchinjaji  wanyama kama ng’ombe, mbuzi na nguruwe .

Wanyama hao wanatakiwa kufikisha katika machinjio maalum inayotambulika kisheria   chini ya maafisa mifugo kwa ajili ya ukaguzi wa nyama yeyote itakayochinjwa kabla ya kusafirishwa kwenda kwa walaji.

Licha ya utaratibu huo kumekuwa na tatizo kubwa la elimu duni kwa wafanyabiashara wa  nyama na badala yake wengi wao wanachinja  wanyama hao majumbani mwao na kuuza bila kupimwa.

Hatua hiyo ni kunahatarisha masiaha ya walaji  ambao huambukizwa magonjwa kutoka kwa wanyama hao bila kujua kama haijathibitishwa na wataalam.

Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia mbuzi na nguruwe wakichinjwa bila kuhusishwa maofisa mifugo huku baadhi yetu tukiwa wa kwanza kununua nyama hiyo bila kujua athari zake baadaye.

Bw. Jamse Yuda, Kaimu Ofisa Kilimo na Mifugo na Ushirika katika Manispaa ya Morogoro anaelezea athari ambazo zinaweza kumpata moja  kwa moja mlaji wa nyama isiyokaguliwa na wataaalam husika.

Anasema mara nyingi nyama ya mbuzi na nguruwe  ukaguzi wake umekuwa mgumu kutokana na jamii kutokuwa na elimu kuhusu athari za uuzaji wa nyama isiyo na kibali cha kuuzwa kutoka  kwa afisa mifugo .

Wafanyabiashara wengi wa nyama hizo wamekuwa na tabia ya kuchinja wanyama hao majumbani ambao kinyume cha sheria bila kuchukuliwa hatua huku waathirika wakubwa wakiwa ni wasafiri wanaonunu nyama wakiamini ipo salama.

Bw. Yuda anasema ofisi yake imekuwa ikijitahidi kuzunguka katika maeneo ambayo yamekuwa yakidaiwa kuchinja bila kufuata taratibu na kuendelea kutoa elimu pamoja na kukamata nyama hizo ili kuokoa maisha ya jamii.Anasema wanyama hao wa damu moto wamekuwa na magonjwa mengi hatari kwa binadamu ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya walaji endapo itakuwa na magonjwa.

Anasema sheria namba 16 ya nyama ya mwaka 2003 inayoambatana na sheria ya magonjwa ya wanyama  namba 17 ya mwaka 2003, sheria namba  10 ya mwaka 2006 na sheria ya uchinjaji namba 19 ya mwaka 2008 pamoja na sheria ngozi namba  18 ya mwaka 2008 zinaelekeza kila kitu kuhusu masuala ya matumizi na tatartibu zilizowekwa kuhusu wanyama hao.

Anasema mfanyabiashara kuchinja mnyama holela bila kufuata taratibu ni kukiuka kwa makusudi sheria hizo zote hivyo afisa mifugo husika hana budi kuchukua hatua za kisheria  dhidi  yake kwa mujibu wa tararibu.

Anasema magonjwa yaliyopo kwa wanyama hao wambayo yanaweza kumuambukiza kwa mlaji moja kwa moja baada ya kula nyama yenye ugonjwa hayo.

“Magonjwa kama TB, Kimeta, Tegu, Minyoo na Homa ya mapafu ya mbuzi (CCP), magonjwa haya ni magonjwa hatari kwa binadamu, ”alisema Bw.  Yuda.

Anasema magonjwa hayo ambayo yanaweza kuambukizwa kwa binadamu kwa kula nyama ya mbuzi aliye na malazi hayo bila kujitambua.

Anasema zipo aina fulani za minyoo hatari kwa binadamu moja kwa moja hivyo ni muhimu kwa wahusika kuzingati kanuni za afya.

“Vile vile kuna mafua ya nguruwe ambayo ni hatari kwa mlaji, “ anasema Bw.Yuda .

Anasema waziri mwenye dhamana amepitisha uboreshaji wa sheria ndogo ya wanyama na kuongeza adhabu kwa wale watakao kiuka sheria .Anasema kwa sasa mtu yeyote atakayekutwa amechinja mnyama nyumbani au sehemu ya biashara bila kupeleka machinjio atapewa adhabu ya faini ya shilingi milioni moja au kifungo cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja.

Kwa upande wake ofisa Mifugo Mkaguzi Bw.  Donath Tilya, anaelezea changamoto  zinazoikabili ofisi ya mifugo katika kutekeleza majukumu yao kuwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti.

Anataja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa usafiri hasa kwa kuzingatia kuwa wanatakiwa kuzunguka maeneo ambayo yamekuwa yakiuzwa nyama kiholela kudhibiti hali hiyo hatari kwa maisha ya watanzania.

Changamoto nyingine ni machinjio chakavu iliyojengwa enzi la mkoloni mwaka 1950, tatizo la maji na umeme ambayo yamekuwa yakichangia  kwa kiasi kikubwa utendaji wao kuwa chini ya kiwango.

“Tatizo kubwa ni fedha za kuboresha machinjio kwa kuwa machinjio yetu ni kongwe sana “anasema Bw. Tilya.
Anawataka wafanyabiashara wa nyama Manispaa ya Morogoro kuwa makini na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na mamlaka husika ili kulinda afya za wateja wao na kuepusha  usumbufu na hasara kwao wakigundulika kwenda kinyume.

Anasema jamii pia inatakiwa kuwa wadadisi  badala ya kujenga tabia ya kununua nyama bila kuhoji kama imekaguliwa na maafisa mifugo.Anaomba ushirikiano kwa wananchi katika Manispaa ya Morogoro na ofisi ya mifugo kwa kutoa taarifa ya wote wanaoonekana kuchinja  nyama kiholela na kuingiza katika soko bila kukaguliwa.

No comments:

Post a Comment